Raia milioni mbili wakimbia Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i23083-raia_milioni_mbili_wakimbia_sudan_kusini
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa wakimbizi wa Sudan Kusini zaidi ya milioni mbili walikimbilia Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka jana kwa ajili ya kutafuta hifadhi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 08, 2017 10:22 UTC
  • Raia milioni mbili wakimbia Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa wakimbizi wa Sudan Kusini zaidi ya milioni mbili walikimbilia Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka jana kwa ajili ya kutafuta hifadhi.

Eric Ngala mmoja wa maafisa wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa kiasi hicho kinahesabiwa kuwa ni idadi kubwa zaidi ya wahajiri kuwahi kushuhudiwa barani Afrika tangu kutokea maangamizi ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Afisa huyo wa UNHCR amesisitiza kuwa sababu kuu iliyowapelekea raia hao wa Sudan Kusini kuihama nchi yao ni vita vya ndani vilivyoikumba nchi hiyo tangu mwezi Julai mwaka jana hadi sasa kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar.

Raia wa Sudan Kusini waliokimbilia Uganda kwa ajili ya hifadhi 

Pande mbili hizo hasimu mwezi Agosti mwaka juzi zilisaini makubaliano ya amani ili kuhitimisha mzozo wa ndani huko Sudan Kusini, hata hivyo pande hizo mwezi Julai mwaka jana zilikiuka makubaliano hayo.  

Itakumbukwa kuwa vita vya ndani vilianza huko Sudan Kusini mwezi Septemba mwaka 2013 ambapo watu zaidi ya elfu kumi wameshauawa na wengine milioni mbili na nusu kuwa wakimbizi katika nchi jirani.