Jan 16, 2017 06:11 UTC
  • Waasi wa zamani wa Machi 23 waingia mashariki mwa Congo

Maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo wamesema kuwa waasi wa zamani wa kundi la Machi 23 wameingia mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa serikali ya Congo, Lambert Mende amesema kuwa baadhi ya waasi wa zamani wa kundi la Machi 23 wamerejea katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo wakitokea Uganda na kukivamia kijiji cha Inshasha.

Mende ameikosoa serikali ya Uganda kwa kuwapa hifadhi waasi hao na kusema kuwa, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo halitamruhusu mtu yeyote mwenye silaha kuingia nchini humo kinyume cha sheria.

Wapiganaji wa makundi ya waasi mashariki mwa Congo

Kijiji cha Inshasha  kiko katika eneo la Rutsuru umbali wa kilomita 55 kaskazini mashariki kwa mji wa Goma ulioko karibu na mpaka wa Congo na Rwanda.

M23 ni kundi la waasi wa Kitutsi lililokuwa likiungwa mkono na nchi za Rwanda na Uganda huko mashariki mwa Congo. Maafisa wa serikali ya nchi hiyo wanazituhumu nchi hizo mbili jirani kuwa zinawapa hifadhi na kuwasaada waasi wa kundi hilo.    

Tags