Wanachama watatu wa Daesh watiwa mbaroni Morocco
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24807-wanachama_watatu_wa_daesh_watiwa_mbaroni_morocco
Askari usalama wa Morocco wamewatia mbaroni wanachama watatu wa kundi la kigaidi la Daesh nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2017 04:13 UTC
  • Wanachama watatu wa Daesh watiwa mbaroni Morocco

Askari usalama wa Morocco wamewatia mbaroni wanachama watatu wa kundi la kigaidi la Daesh nchini humo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imetangaza kuwa wanachama watatu wa kundi la kigaidi la Daesh waliotiwa mbaroni walikuwa na lengo la kushambulia maeneo mbalimbali ya umma, hoteli na vituo vya biashara nchini humo.

Magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imeongeza kuwa, wanachama hao watatu wa Daesh wamekamatwa kutokana na taarifa za kiusalama walizopatiwa na mamluki wenye mfungamano na kundi jingine la kigaidi waliokamatwa siku kadhaa zilizopita katika miji kadhaa ya Morocco. Morocco imeshakumbwa kwa mara kadhaa na kundi la kigaidi la Daesh na mara hii magaidi hao walikuwa wameulenga mji wa Marakesh unaopatikana kusini magharibi mwa nchi hiyo.