Libya yakanusha tuhuma za Rais wa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2740-libya_yakanusha_tuhuma_za_rais_wa_tunisia
Msemaji wa serikali ya Libya amekanusha madai ya Rais wa Tunisia kuwa nchi hiyo inazalisha magaidi wanaofanya mashambulizi nchi nyingine.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 09, 2016 10:54 UTC
  • Libya yakanusha tuhuma za Rais wa Tunisia

Msemaji wa serikali ya Libya amekanusha madai ya Rais wa Tunisia kuwa nchi hiyo inazalisha magaidi wanaofanya mashambulizi nchi nyingine.

Shirika la habari la IRIB limemnukuu Hatem al Arabi akisema hayo leo na kukanusha tuhuma za Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia aliyedai kuwa Libya inazalisha magaidi wanaofanya mauaji na jinai katika nchi nyingine.

Al Arabi amesema, madai hayo hayastahiki kutolewa na mtu kama Rais wa Tunisia na bila ya shaka yoyote wananchi wa Libya na Tunisia hawakufurahishwa na matamshi hayo.

Amesisitiza kuwa, usalama wa mataifa yote jirani na Libya uko hatarini na kwamba nchi hiyo haizalishi magaidi. Amesema, kutokana na kuzembea jamii ya kimataifa kuisaidia nchi hiyo kumepelekea kuwa maficho mazuri ya makundi ya kigaidi.

Aidha amesisitiza kuwa, sehemu kubwa ya magaidi walioko Libya ni raia wa Tunisia na wananchi wa Libya wanateseka hivi sasa kwa ukosefu wa amani kutokana na ugaidi huo wa raia wa Tunisia, lakini pamoja na yote hayo serikali na wananchi wa Libya hailihesabu taifa la Tunisia kuwa ndilo linalosababisha ukosefu wa amani huko Libya, bali Libya inailaumu jamii ya kimataifa kwa kufanya uzembe katika miaka ya hivi karibuni na ndilo jambo lililopelekea kuongezeka magenge ya kigaidi nchini humo.