Zuma ayataja maandamano ya Afrika Kusini dhidi yake kuwa ni ya kibaguzi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27588-zuma_ayataja_maandamano_ya_afrika_kusini_dhidi_yake_kuwa_ni_ya_kibaguzi
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini leo ameyataja maandamano ya wiki iliyopita nchini humo ya kumshinikiza ajiuzulu kuwa ni ya kibaguzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 10, 2017 10:26 UTC
  • Zuma ayataja maandamano ya Afrika Kusini dhidi yake kuwa ni ya kibaguzi

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini leo ameyataja maandamano ya wiki iliyopita nchini humo ya kumshinikiza ajiuzulu kuwa ni ya kibaguzi.

Makumi ya maelfu ya wananchi Ijumaa iliyopita waliandamana katika miji mbalimbali ya Afrika Kusini kudhihirisha hasira zao kutokana na kashfa mbalimbali za ubadhirifu, ukosefu wa ajira na kuzorota uchumi chini ya utawala wa Rais Zuma. Hatua ya Zuma ya kumfuta kazi Pravin Gordhan Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini aliyekuwa akiheshimika nchini humo imeibua upinzani na malalamiko mapya ya wananchi na kutoka kwa shakhsia wa ngazi ya juu wa chama tawala ANC, akiwemo Makamu wa Rais.

Maandamano dhidi ya Rais Zuma  

Rais Jacob Zuma amesema kuwa maandamano ya wiki iliyopita yamedhihirisha kuwa ubaguzi upo huko Afrika Kusini. Amesema mabango na maberamu yaliyobebwa na waandamanaji yalidhihirisha imani ambazo amesema walidhani zilishatokomezwa, huku mabango mengine yakiwa yamechorwa raia weusi na kuwaonyesha kuwa ni nyani.