Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini awasili Tanzania kwa ziara rasmi
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, aliwasili nchini Tanzania jioni ya jana kwa ziara ya kikazi.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Dar es Salaam inasema Rais Zuma atakuwa nchini humo kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko wa rais mwenzake John Magufuli.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ziara ya Rais Zuma nchini Tanzania inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Kadhalika katika ziara hiyo rais huyo wa Afrika Kusini anatarajiwa kushiriki mkutano wa wafanyabiashara, kuzindua jengo la Ubalozi wa Afrika Kusini na kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uhusiano kati ya Pretoria na Dar es Salaam ni wa muda mrefu, tangu nchi hizo zilipokuwa zikipigania uhuru.