Magaidi wa Al Shabab waua afisa wa utawala Kenya
(last modified Tue, 16 May 2017 14:13:09 GMT )
May 16, 2017 14:13 UTC
  • Magaidi wa Al Shabab waua afisa wa utawala Kenya

Watu wanaoaminika kuwa magaidi wa kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka Somalia wameingia katika eneo la mpakani kaskazini mashariki mwa Kenya na kumuua afisa mmoja wa utawala nchini humo.

Taarifa zinasema magaidi wanne waliokuwa wamevalia sare za kijeshi waliingia katika kaunti ya Mandera, karibu na mpaka wa Somalia na kumpiga risasi na kumuua chifu aliyetambuliwa kwa jina la Omar Jillo.

Mkuu wa Polisi Kaskazini Masahriki mwa Kenya Edward Mwamburi ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa waliotekelza hujuma hiyo wanashukiwa kuwa magaidi wa Al Shabab kwani walitorekea nchini Somalia.

Kuanzia mwaka 2012, kundi la al-Shabab limekuwa sehemu ya mtandao wa kigaidi wa al-Qaidah nchini Somalia. Baada ya wanachama wa kundi la ash-Shabab kushindwa kupambana na askari wa nchi hiyo, wamekuwa wakitelekeza hujuma na uharibifu katika maeneo mbali mbali ya Kenya hasa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kenya ina maelfu ya wanajeshi katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kwa shabaha ya kuwaangamiza wanamgambo wa al Shabab na kuimarisha usalama kama sehemu ya kuijenga upya Somalia baada ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoirudisha nyuma kimaendeleo nchi hiyo.

 

Tags