AU yataka kupewa nafasi zaidi katika Baraza la Usalama
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31288-au_yataka_kupewa_nafasi_zaidi_katika_baraza_la_usalama
Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amezitaka nchi za bara hilo kuungana kwa ajili ya kuinua juu nafasi na hadhi ya Afrika na kuimarisha uwakilishi wake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jul 03, 2017 08:32 UTC
  • AU yataka kupewa nafasi zaidi katika Baraza la Usalama

Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amezitaka nchi za bara hilo kuungana kwa ajili ya kuinua juu nafasi na hadhi ya Afrika na kuimarisha uwakilishi wake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Naibu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Thomas Kwesi Quartey amesema kuwa, muundo wa sasa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unaakisi sauti za dunia ya baada ya Vita vya Pili vya Dunia na kwamba tangu wakati huo dunia imebadilika na miongoni mwa mabadiliko hayo ni kuongezeka uwezo na nguvu ya Afrika katika nyanja za kimataifa; hivyo kuna ulazima wa kuimarishwa zaidi ushiriki na uwakilishi wa bara hilo katika taasisi za kimataifa. 

Mkutano wa Umoja wa Afrika

Viongozi wa nchi za Afrika wanakutana leo na kesho katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na wanatarajiwa kupasisha mapendekezo yanayohusiana na suala la kupewa viti viwili vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mwaka 2005 nchi za Afrika zilichukua msimamo mmoja kwa ajili ya kufanyika marekebisho katika muundo wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na bara hilo kupewa viti viwili vya kudumu na haki ya kura ya veto katika Baraza la Usalama,