Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Kenya na ishara za kukomaa demokrasia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33873-uamuzi_wa_mahakama_kuu_ya_kenya_na_ishara_za_kukomaa_demokrasia
Mahakama ya Juu ya Kenya imetengua matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita nchini humo na kumpa ushindi Rais wa sasa wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Sep 02, 2017 05:24 UTC
  • Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Kenya na ishara za kukomaa demokrasia

Mahakama ya Juu ya Kenya imetengua matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita nchini humo na kumpa ushindi Rais wa sasa wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.

Jopo la majaji sita wa Kenya, na kwa uamuzi wa wengi, Ijumaa ya jana lilisema lilmegundua kuwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haikuweza kuendesha zoezi la uchaguzi kulingana na Katiba na Sheria za Uchaguzi. 

Majaji wa Mahakama Kuu ya nchi hiyo wamesema kuwa tume hiyo haikuendesha zoezi hilo kwa njia sahihi na wametaka ufanyike tena katika kipindi cha siku 60 sijazo. Majaji wa mahakama hiyo wamewakosoa maafisa wa Tume ya Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa wameshindwa, kuzembea au kuacha kuendesha zoezi la uchaguzi kwa mujibu wa sheria. 

Hii ni mara ya kwanza nchini Kenya bali barani Afrika uchaguzi wa rais kubatilishwa na mahakama. Kuhusu suala hilo kinara wa upinzani Raila Odinga ameitaja Ijumaa ya jana kuwa ni siku ya kihistoria na kusisitiza kuwa: “Leo tunasherehekea sikukuu ya Eid lakini pia tuna sherehe nyingine ambayo Mahakama imetupatia.” Amesema kuwa, uamuzi wa Mahakama Kuu umeipa heshima Kenya katika ujenzi wa demokrasia. 

Image Caption

Kenya ina historia ya machafuko na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu. Mwaka 2007 nchi hiyo ilikumbwa na machafuko makubwa yaliyokaribia kuitumbukiza katika vita vya kikabila na mauaji ya kimbari baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliompa ushindi Mwai Kibaki. Zaidi ya watu 1200 waliuawa katika machafuko hayo na malaki ya wengine wakalazimika kuwa wakimbizi. 

Tangu mwanzoni mwa zoezi la uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika tarehe 8 Agosti, kambi ya upinzani ilitahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea udanganyifu na kuchezewa kompyuta zilizotumiwa kuhesabu kura za wananchi. Vilevile kambi ya upinzani ilisisitiza kuwa, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inakipendelea chama tawala cha Jubilee na kutoa wito wa kufanyiwa mabadiliko tume hiyo.

Wakati wa zoezi hilo pia muungano wa upinzani cha NASA ulidai kuwa baadhi ya kura za wananchi zimeibiwa na kwamba mfumo wa kompyuta uliotumiwa kwa ajili ya kura za wananchi umedukuliwa.

Vyovyote vile itakavyokuwa, uamuzi wa Mahakama Kuu ya Kenya wa kutengua uchaguzi wa rais umetoa ujumbe kadhaa kwa nchi mbalimbali hususan za Afrika ambazo viongozi wa baadhi ya nchi hizo wamekuwa waking'ang'ania madaraka kwa kutumia njia zote zinazowezekana ikiwa ni pamoja na kubadilisha katiba ya nchi kwa maslahi ya mtu binafsi.  

Rais Joseph kabila wa Congo DR anang'ang'ania madaraka licha ya kipindi cha utawala wake kumalizika

Kama alivyosema kinara wa upinzani nchini Kenya Bwana Raila Odinga “Uamuzi wa Mahakama Kuu ya nchi hiyo umetoa sura mpya na umetuma ujumbe wa kukomaa demokrasia nchini humo na Afrika.

Vilevile uamuzi wa Mahakama Kuu ya Kenya umeonesha kuwa, Mahakama zinaweza kuwa na uhuru na kusimama dhidi ya nguvu za marais barani Afrika.

Somo jingine linalopatikana katika kadhia hii ni lile la kuheshimu maamuzi ya taasisi za juu kama Mahakama Kuu na kujiepusha na ghasia na machafuko pale maamuzi hayo yanapokwenda kinyume na matakwa na maslahi ya watawala. Somo hilo limepatikana kutokana na msimamo wa Rais Uhuru Kenyatta wa kuheshimu uamuzi wa majaji wa Mahakama Kuu uliomyang'anya ushindi licha ya kwamba hakubaliani nao.