AU yapongeza uamuzi wa mahakama ya juu Kenya kubatilisha uchaguzi wa rais
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33936-au_yapongeza_uamuzi_wa_mahakama_ya_juu_kenya_kubatilisha_uchaguzi_wa_rais
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU amekaribisha uamuzi wa mahakama ya juu nchini Kenya wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 04, 2017 22:07 UTC
  • AU yapongeza uamuzi wa mahakama ya juu Kenya kubatilisha uchaguzi wa rais

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU amekaribisha uamuzi wa mahakama ya juu nchini Kenya wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais nchini humo.

Rais Alpha Condé wa Guinea ambaye ni mwenyekiti wa hivi sasa Umoja wa Afrika alisema hayo jana Jumatatu katika taarifa yake na kuongeza kuwa, hatua ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ya kukubali uamuzi wa mahakama hiyo, inathibitisha kukomaa kidemokrasia bara la Afrika. Katika ripoti hiyo pia imeeleza kuwa Umoja wa Afrika inaupa umuhimu maalumu mwenendo wa kisiasa nchini Kenya na kwa mara nyingine tena amewataka raia na viongozi wa kisiasa wa nchi hiyo kujizuia na kujihisi majukumu kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi mpya.

Rais Alpha Condé wa Guinea, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika

Matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Kenya uliofanyika tarehe nane Agosti, yalifutwa siku ya Ijumaa iliyopita na mahakama ya juu ya nchi hiyo baada ya upande wa upinzani kuwasilisha malalamiko kwamba kulikuwa na uchakachuaji katika mchakato wa kuhesabu kura kwa maslahi ya Rais Kenyatta. Uamuzi huo wa Mahakama ya Juu ya Kenya umeibua mchuano mpya kati ya  Kenyatta mwenye miaka 55, na hasimu wake Odinga aliye na miaka 72, huku mivutano ikiongezeka kati ya kambi mbili hizo hasimu.