Al-Shabab washambulia mji wa Kismayo watatu wauawa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i3403-al_shabab_washambulia_mji_wa_kismayo_watatu_wauawa
Watu watatu wameripotiwa kuuawa na wengine sita kujeruhiwa kufuatia shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi la ash-Shabab katika eneo lililo karibu na mji wa Kismayo nchini Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 19, 2016 23:35 UTC
  • Al-Shabab washambulia mji wa Kismayo watatu wauawa

Watu watatu wameripotiwa kuuawa na wengine sita kujeruhiwa kufuatia shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi la ash-Shabab katika eneo lililo karibu na mji wa Kismayo nchini Somalia.

Shambulio hilo limehusu kiwanda cha makaa ya mawe cha eneo la Burjabu lililo umbali wa kilometa 40 magharibi mwa mji wa Kismayo. Kwa mujibu wa mashuhuda, wahanga wa shambulio hilo ni wafanyakazi wa kiwanda hicho, na kwamba walikumbwa na hujuma hiyo wakati walipokuwa wakikata miti katika eneo hilo. Habari zinasema kuwa, wanamgambo wa kundi hilo la kitakfiri walikuwa wakiingiza pato kubwa la fedha kutokana na biashara ya makaa ya mawe katika mji wa Kismayo wenye umuhimu mkubwa baada ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Ni vyema kuashiria kuwa, licha ya kundi la ash Shabab kufurushwa kutoka katika miji muhimu ya nchi hiyo, lakini linaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo tofauti ya nchi hiyio ya Pembe ya Afrika.