Wanawake waandamana Mali kupinga kuwepo majeshi ya kigeni nchini humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35197-wanawake_waandamana_mali_kupinga_kuwepo_majeshi_ya_kigeni_nchini_humo
Wanawake wa mji wa Kidal ulioko kaskazini mwa Mali wameandamana kulalamikia na kupinga kuwepo majeshi ya kigeni hususan ya Ufaransa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 03, 2017 22:52 UTC
  • Wanawake waandamana Mali kupinga kuwepo majeshi ya kigeni nchini humo

Wanawake wa mji wa Kidal ulioko kaskazini mwa Mali wameandamana kulalamikia na kupinga kuwepo majeshi ya kigeni hususan ya Ufaransa nchini humo.

Katika maandamano yao hayo, wanawake hao wamelaani operesheni ya msako wa nyumba hadi nyumba iliyofanywa na askari wa Ufaransa na kutiwa nguvuni watu kadhaa katika mji huo na kutaka vikosi vya majeshi ya kigeni hasa vya Ufaransa viondoke nchini humo.

Ripoti zinaeleza kuwa siku ya Jumamosi usiku askari wa Ufaransa walifanya msako wa nyumba hadi hadi nyumba katika mji wa Kidal kupitia operesheni ya kijeshi ya Barkhane na kuwatia mbaroni raia saba.

Askari wa Ufaransa wakiwa katika doria mjini Kidal, kaskazini mwa Mali

Katika maandamano ya wanawake wa mji wa Kidal, waandamanaji wamelaani utumiaji mada za miripuko uliofanywa na askari wa Ufaransa na uchomaji moto kwa makusudi vyombo vya usafiri katika mji huo.

Mapinduzi ya kijeshi yalitokea nchini Mali mwaka 2012 na kufuatiwa na machafuko na kupata nguvu makundi ya wabeba silaha.

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa Ufaransa wamekuwepo nchini humo tangu mwaka 2013 lakini hadi sasa wameshindwa kukomesha machafuko na kuzima vitisho vya ugaidi nchini humo.../