Kikao cha nchi jirani na Libya huko Tunisia
-
Nchi jirani na Libya
Kikao cha nchi jirani na Libya kimefanyika huko Tunisia. Kanali ya televisheni ya al Aalam imeripoti kuwa kikao cha nchi jirani na Libya kimefanyika leo katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia.
Kikao hicho cha nchi jirani na Libya kimechunguza mchakato wa mazungumzo ya Libya na njia za kuunga mkono jitihada za kisiasa huko Libya. Kikao hicho vile vile kimejadili suala la kuiwezesha serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya kutekeleza majukumu yake na pia kuunga mkono juhudi kwa ajili ya kurejesha amani na uthabiti nchini humo.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia, Libya, Algeria, ,Misri, Sudan, Chad, Niger na pia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League na wawakilishi wa Umoja wa Afrika na Ulaya pamoja na Mwenyekiti wa ujumbe maalumu wa kimataifa kuhusu Libya wameshiriki kwenye kikao hicho.