Maelfu ya Watogo waandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35281-maelfu_ya_watogo_waandamana_dhidi_ya_rais_wa_nchi_hiyo
Maelfu ya raia wa Togo wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lome dhidi ya Rais Faure Gnassingbé wa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 06, 2017 01:11 UTC
  • Maelfu ya Watogo waandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo

Maelfu ya raia wa Togo wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lome dhidi ya Rais Faure Gnassingbé wa nchi hiyo.

Waandamanaji katika mandamano hayo ya saba dhidi ya serikali ya Togo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, wanamtaka Faure Gnassingbé ang'atuke madarakani.

Waandamanaji hao pia wametaka kurejeshwa katiba ya mwaka 1982 ambayo kwa mujibu wake Faure Gnassingbé haruhusiwi kugombea tena kiti cha Rais wa Togo.

Image Caption

Vilevile wamepinga mikakati inayofanywa na serikali ya Lome ya kuitisha kura ya maoni kwa ajili ya kupasisha marekebisho ya katiba ya nchi hiyo. Marekebisho hayo ambayo yanapingwa na vyama vya siasa vya upinzani, yatamruhusu Faure Gnassingbé kugombea tena kiti cha rais wa Togo mara mbili zaidi hadi mwaka 2020.

Kiongozi wa zamani wa Togo Gnassingbé Eyadéma ambaye alikuwa baba wa rais wa sasa wa nchi hiyo aliiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30 hadi alipofariki dunia mwaka 2005. Kiongozi huyo pia alidumisha utawala wake kwa kuifanyia marekebisho katiba ya Togo.