Harakati za Israel za kutaka kupenya katika Umoja wa Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35365-harakati_za_israel_za_kutaka_kupenya_katika_umoja_wa_afrika
Balozi wa Palestina nchini Ethiopia amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya harakati za kutaka kupenya katika Umoja wa Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 07, 2017 23:12 UTC
  • Harakati za Israel za kutaka kupenya katika Umoja wa Afrika

Balozi wa Palestina nchini Ethiopia amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya harakati za kutaka kupenya katika Umoja wa Afrika.

Nasir Abu Jaish, balozi wa Palestina mjini Addis Ababa Ethiopia ameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umo mbioni kufanya juhudi za kukubaliwa kama mtazamaji katika Umoja wa Afrika AU.

Balozi huyo wa Palestina nchini Ethiopia amesema kuwa, ujumbe wa utawala huo ghasibu umo katika nchi hiyo ya Kiafrika yalipo makoa makuu ya Umoja wa Afrika ili kukabidhi ombi lake la kukubaliwa kuwa mtazamaji katika jumuiya hiyo kubwa zaidi barani Afrika.

Kwa mujibu wa Nasir Abu Jaish ni kuwa, katika kipindi cha miaka minne iliyopita, utawala haramu wa Israel umeomba zaidi ya mara kumi kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika, lakini kila mara ombi lake hilo lilikataliwa.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni

Hayo yanajiri katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kuakhirishwa mkutano wa pamoja kati yake na Umoja wa Afrika uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi huu wa Oktoba.

Inaelezwa kuwa, kumekuwa na upinzani mkali dhidi ya hatua za utawala wa Kizayuni za kutaka kukubaliwa kama mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika.

Afrika Kusini imekuwa mstari wa mbele miongoni mwa nchi zinazokabiliana na upenyaji na ushawishi wa Israel barani Afrika. Nchi nyingine ni Morocco, Algeria, Tunisia na Mauritania.

Nchi hizo zimekuwa zikipinga Israel kukubaliwa kama mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrtika kutokana na siasa za ukandamizaji na mauaji za utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.