UN yaeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya wakimbizi wa Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i35977-un_yaeleza_wasiwasi_wake_kuhusu_hali_ya_wakimbizi_wa_sudan_kusini
Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya wakimbizi wa Sudan Kusini walioko katika mji mkuu wa nchi jirani ya Sudan, Khartoum.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 27, 2017 04:13 UTC
  • UN yaeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya wakimbizi wa Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya wakimbizi wa Sudan Kusini walioko katika mji mkuu wa nchi jirani ya Sudan, Khartoum.

Kamishna wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa amesema kuwa, katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita polisi ya Sudan imeharibu makazi ya wakimbizi wa Sudan Kusini mjini Khartoum na kuwapeleka baadhi yao kwenye maeneo mengine bila ya utaratibu na maandalizi sahihi. 

Ripoti ya hivi karibuni inasema kuwa makazi 220 ya wakimbizi wa Sudan Kusini yameharibiwa katika eneo la Daru Salaam mjini Khartoum. Ripoti hiyo inasema wakimbizi karibu elfu mbili walikuwa wakiishi katika eneo hilo. 

Wakimbizi zaidi ya laki nne na nusu wa Sudan Kusini wamekimbilia nchi jirani ya Sudan tangu mwaka 2013 kwa kuhofia ukatili na machafuko yanayoendelea katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. 

Serikali ya Sudan inasema wakimbizi milioni moja kutoka Sudan Kusini wameomba hifadhi nchini humo.