Kutolewa kibali kwa ajili ya kufanyika uchunguzi kuhusu machafuko nchini Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36331-kutolewa_kibali_kwa_ajili_ya_kufanyika_uchunguzi_kuhusu_machafuko_nchini_burundi
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa kibali cha kuruhusu kufanywa uchunguzi kuhusu machafuko na uwezekano wa kutendwa jinai dHidi ya binadamu huko Burundi huku serikali ya nchi hiyo ikipinga uamuzi huo na kusisitiza kuwa Burundi kamwe haitashirikiana na mahakama hiyo.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Nov 12, 2017 01:03 UTC
  • Kutolewa kibali kwa ajili ya kufanyika uchunguzi kuhusu machafuko nchini Burundi

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa kibali cha kuruhusu kufanywa uchunguzi kuhusu machafuko na uwezekano wa kutendwa jinai dHidi ya binadamu huko Burundi huku serikali ya nchi hiyo ikipinga uamuzi huo na kusisitiza kuwa Burundi kamwe haitashirikiana na mahakama hiyo.

Aimee Laurentine Kanyana Waziri wa Sheria wa Burundi ameashiria kuwa nchi hiyo ilijiondoa katika mahakama ya ICC tangu Oktoba 27 na kwamba serikali ya Bujumbura haina taarifa kuhusu uamuzi wa taasisi hiyo kwani hivi sasa Burundi haina uhusiano na mahakama hiyo wala maamuzi inayochukua.  

Tarehe 27 Oktoba mwaka huu, Burundi iliwasilisha ombi la kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa Katibu Mkuu wa wakati huo wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon; ombi ambalo limekubaliwa baada ya kupita karibu mwaka mmoja na kuifanya Burundi kuwa nchi ya kwanza  kujiondoa ndani ya ICC. Pamoja na hayo yote, kuondoka Burundi katika ICC haijawa sababu ya kufumbiwa macho na mahakama hiyo jinai zinazodaiwa kutokea huko Burundi.  

Burundi ilikumbwa na mgogoro wa kisiasa na machafuko yaliyozusha mapigano ya umwagaji damu tangu kufanyika uchaguzi uliopingwa kikamilifu na wapinzani na kuzusha mabishano makubwa mwaka 2015. Hata hivyo uchaguzi ulifanyika na Rais Pierre Nkurunziza amebakia madarakani.  Wapinzani wa Nkurunziza wanaamini kwamba uchaguzi huo wa mwaka 2015 ulikuwa ni kinyume na katiba na masharti ya makubaliano ya amani ambayo yalihitimisha vita vya ndani huko Burundi. Wapinzani hao wanasema kuwa Rais anapasa kuwepo madarakani kwa mihula miwili ya miaka minne minne na Nkurunziza alishiriki katika uchaguzi wa mwaka 2015 kinyume na katiba. 

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundii aliyekataa kuondoka madarakani  

Hata kama kupambana moto mapigano huko Burundi kulizipelekea nchi za eneo kufanya juhudi za kumuainisha msuluhishi wa kikanda ili kuupatia ufmbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo, lakini wapinzani wa Burundi walitaka kujiuzulu Nkurunziza huku chama tawala kikiamini kuwa Nkurunziza yupo madarakani kwa mujibu wa sheria. Ndio maana baada ya kupita zaidi ya miaka mwili na licha ya kufanyika juhudi za kimataifa na kieneo kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgopgoro wa kisiasa huko Burundi lakini hadi kufikia sasa juhudi hizo zimeshindwa kuzaa matunda. 

Pamoja na kuwa hivi sasa hali ya mambo  huko Burundi inaonekana kuwa tulivu na shwari, lakini ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa askari usalama wa Burundi wamekuwa wakitumia mabavu kuzusha machafuko, kutekeleza mauaji  dhidi ya wapinzani.  Aidha ripoti ilkiyotolewa huko nyuma na Umoja wa Mtaifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na askari usalama huko Burundi imekuwa chanzo cha kuongezeka mivutano kati ya serikali ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa. Ripoti mbalimbali zinaonyesha mamia ya matukio ya kunyongwa watu, kutiwa mbaroni kiholela, mateso na udhalilishaji wa kijinsia vilivyojiri huko Burundi. Kuhusiana na suala hilo, Babar Baloch Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuwa: idadi ya wakimbizi huko Burundi itafikia zaidi ya nusu milioni ifikapo mwishoni mwaka mwaka huu wa 2017 iwapo hali ya kisiasa nchini haitaboreka. 

Babar Baloch, Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya UN 

Licha ya kutolewa ripoti hizo, viongozi wa Burundi kwa upande wao wanakanusha kujiri vitendo vyovyote vya utumiaji mabavu  nchini humo. Venuste Muyabaga mwakilishi wa masuala ya kisheria wa taasisi ya kiraia ya Burundi anasema kuhusu suala hilo kuwa: Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa katika ripoti hizo wametegemea matamshi ya baadhi ya wahalifu waliotorokea nje ya mipaka ya nchi hiyo. 

Katika mazingira hayo, haifahamiki iwapo ombi hilo la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na kutolewa kibali cha kufanyika uchunguzi kuhusu machafuko huko Burundi kwa kiasi gani vitaweza kupunguza mzozo wa kisiasa na machafuko huko Burundi.