Waasi wa Darfur watangaza kusitisha vita kwa miezi miwili
Makundi matatu ya waasi wa eneo la Darfur huko magharibi mwa Sudan yametangaza usitishaji vita wa miezi miwili hadi tarehe 31 Januari mwaka 2018.
Viongozi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan, Harakati ya Usawa na Uadilifu na kundi la SLM la Mini Minawi wametangaza kuwa wamesitisha vita na uhasama na serikali kuu ya Sudan.
Makundi hayo yametangaza kuwa yatasitisha vita na mapigano ya aina zote isipokuwa kwa ajili ya kujilinda.
Baada ya tangazo hilo, maafisa wa serikali ya Khartoum wanafanya jitihada za kuzidisha misaada ya kibinadamu, kuwasaidia raia na watu walioathiriwa na vita katika eneo hilo.

Sudan imekuwa katika vita na makundi kadhaa ya waasi katika majimbo ya Kordofan Kusini na Bluu Nile tangu mwaka 2011. Mwaka 2013 pia nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika eneo la Darfur ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha wengine kuwa wakimbizi.