Al-Shabaab yadai kuua askari kadhaa wa Somalia, akiwemo kamanda
(last modified Mon, 04 Dec 2017 02:39:33 GMT )
Dec 04, 2017 02:39 UTC
  • Al-Shabaab yadai kuua askari kadhaa wa Somalia, akiwemo kamanda

Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) linadai kuwa limeua askari kadhaa wa Jeshi la Ulinzi la Somalia SNA akiwemo kamanda wa ngazi za juu wa jeshi hilo.

Katika taarifa iliyochapishwa jana Jumapili katika mitandao inayofungana na al-Shabaab, kundi hilo la ukufurishaji limedai kuwa mbali na kuua 'idadi kubwa' ya askari wa Somalia, limemuangamiza pia Kanali Mohamed Rageh, kamanda wa ngazi za juu wa SNA.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanajeshi hao waliuawa baada ya msafara wa magari yao kushambuliwa, ulipokuwa ukitoka Mogadishu ukielekea mji wa Jowhar, makao makuu ya eneo la Shabelle ya Kati.

Vyanzo vingine vya habari vimetangaza kuwa wanamgambo kadhaa wa genge la al-Shabaab wameuawa katika shambulizi hilo la jana Jumapili.

Rais Mohammed Abdullahi Farmajo wa Somalia na makamanda wa jeshi

Hii ni katika hali ambayo, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, Francisco Madeira hivi karibuni alisema kuwa Kikosi cha Askari wa Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM kimeanza kupunguza idadi ya askari wake nchini humo na kwamba kufikia tarehe 31 Disemba askari 1000 wa kikosi hicho watakuwa wameondoka katika ardhi ya Somalia.

Kikosi hicho ambacho kiliundwa kupitia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kimekuwa kikiisaidia serikali ya Somalia kupambana na magaidi wa kundi la al Shabab tangu mwaka 2007. 

Tags