Russia yakadhibisha kumuunga mkono kamanda wa jeshi la Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37659-russia_yakadhibisha_kumuunga_mkono_kamanda_wa_jeshi_la_libya
Balozi wa Russia nchini Libya amekadhibisha madai kwamba nchi yake inamuunga mkono kamanda wa jeshi la taifa la Libya na kuyataja madai hayo kuwa ya uongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 16, 2017 00:16 UTC
  • Russia yakadhibisha kumuunga mkono kamanda wa jeshi la Libya

Balozi wa Russia nchini Libya amekadhibisha madai kwamba nchi yake inamuunga mkono kamanda wa jeshi la taifa la Libya na kuyataja madai hayo kuwa ya uongo.

Ivan Milotkov amekadhibisha habari kwamba Moscow inamuunga mkono Meja Jenerali Khalifa Haftar na kueleza kuwa, Moscow imesisitiza mara kadhaa kuwa haiuungi mkono upande wowote wa kisiasa huko Libya. 

Khalifa Haftar, kamanda wa Jeshi la Taifa la Libya  

Molotkov ameongeza kuwa, Russia haitaki kuupuza upande wowote huko Libya bali inatoa wito kwa pande zote kuketi kwenye meza ya mazungumzo ya kitaifa ili kufikia mwafaka kwa maslahi ya nchi.  

Balozi wa Russia nchini Libya pia amesema Moscow iko tayari kwa ajili ya kuiondolea Libya vikwazo vya silaha iwapo kutaundwa kikosi cha pamoja cha ulinzi nchini humo na kusisitiza kuwa, Russia ina shaka kwamba silaha kutoka nje zinaangukia katika mikono ya magaidi nchini Libya.