Uchumi wa Afrika Kusini mwa Sahara kustawi kwa asilimia 3.1 mwaka 2018
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43376-uchumi_wa_afrika_kusini_mwa_sahara_kustawi_kwa_asilimia_3.1_mwaka_2018
Benki ya Dunia imepandisha makadirio yake kuhusu ustawi wa uchumi wa Afrika kuwa asilimia 3.1 mwaka 2018, baada ya uchumi wa kanda hiyo kudidimia kwa miaka mitatu kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 20, 2018 02:56 UTC
  • Uchumi wa Afrika Kusini mwa Sahara kustawi kwa asilimia 3.1 mwaka 2018

Benki ya Dunia imepandisha makadirio yake kuhusu ustawi wa uchumi wa Afrika kuwa asilimia 3.1 mwaka 2018, baada ya uchumi wa kanda hiyo kudidimia kwa miaka mitatu kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa kimataifa.

Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema ukuaji wa uchumi unatarajiwa kufikia asilimia 3.6 katika mwaka 2019 na asilimia 3.7 katika mwaka 2020.

Ripoti inasema, makadirio ya ongezeko hilo yanatarajiwa kuvutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja kutoka China na nchi zilizoendelea, na kupanua biashara ya kimataifa.

Bandari ya Mogadishu

Hata hivyo benki hiyo pia imeonya kuwa, kukosekana mabadiliko katika muundo wa uchumi kunaweza kuzuia ongezeko la pato la ndani la Afrika.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa,  Nigeria, Afrika Kusini na Angola zinatazmiwa kushuhudia ustawi wa uchumi hatua kwa hatua huku uchumi wa Afrika Magharibi ukiimarika; nazo nchi za Afrika Magharibi na Afrika Mashariki pia zitashuhudia kuboreka uchumi.