Madaktari Congo DR waanza mgomo wakidai mishahara yao
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43592-madaktari_congo_dr_waanza_mgomo_wakidai_mishahara_yao
Madaktari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameanza mgomo wakidai mishahara yao iliyocheleweshwa,
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 24, 2018 12:00 UTC
  • Madaktari Congo DR waanza mgomo wakidai mishahara yao

Madaktari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameanza mgomo wakidai mishahara yao iliyocheleweshwa,

Jumuiya ya Madaktari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, madaktari 3,500 wa hospitali za umma ambao hawajapokea mishahara yao kwa kipindi cha miaka minne sasa wameanza mgomo wa kipindi kisichojulikana kwa shabaha ya kuilazimisha serikali ili itatue suala hilo.

Jumuiya hiyo imesisitiza kuwa, madaktari hao wanafanya mgomo kulalamikia hatua ya serikali ya Kinshasa ya kutotekeza ahadi yake iliyoitoa Disemba mwaka jana. 

Madaktari wa hospitali za serikali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanataka kuboreshwa hali ya maisha ya madaktari ambao hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi cha miaka minne na kupandishwa vyeo. 

Kwa sasa madaktari walioajiriwa mwaka 2000 nchini Congo DR wanalipwa mishahara sawa na wale walioajiriwa mwaka huu wa 2018.

Kutolipwa mishahara ya madaktari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumetatiza hali ya kimaisha ya madaktari hao na familia zao.