ICC yasisitiza kuchunguzwa jinai za kivita zilizofanywa Kongo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44104-icc_yasisitiza_kuchunguzwa_jinai_za_kivita_zilizofanywa_kongo_dr
Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ametaka uanzishwe uchunguzi kuhusu ripoti za ukiukaji haki za binadamu uliofanywa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupandishwa kizimbani waliohusika na vitendo hivyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 05, 2018 22:05 UTC
  • ICC yasisitiza kuchunguzwa jinai za kivita zilizofanywa Kongo DR

Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ametaka uanzishwe uchunguzi kuhusu ripoti za ukiukaji haki za binadamu uliofanywa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupandishwa kizimbani waliohusika na vitendo hivyo.

Fatou Bensouda ameashiria kugunduliwa na kuorodheshwa na Umoja wa Mataifa makumi ya makaburi ya halaiki katika eneo la Kasai katikati mwa Kongo DR na kusisitizia ulazima wa kuanzishwa uchunguzi na kufunguliwa mashtaka waliohusika na jinai hizo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, hadi sasa kuna mafaili kadhaa ya tuhuma za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo yameorodheshwa na kufikishwa kwenye mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo.

Idadi kubwa ya watu wameuawa katika eneo la Kasai tangu mwezi Julai 2016 hadi sasa kufuatia kushadidi mapigano kati ya waasi na vikosi vya jeshi la serikali.

Tangu miaka 20 nyuma hadi sasa, mapigano, machafuko na hali ya mchafukoge inatawala katika maeneo ya kati, mashariki na kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.../