Rwanda yachukua hatua kali zaidi dhidi ya vyombo vya plastiki + Sauti
Jun 05, 2018 13:26 UTC
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya mazingira, serikali ya Rwanda imepiga hatua nyingine mbele ya kukomesha matumizi ya aina yoyote ya vifaa vya plastiki kwa sababu vinahatarisha maisha ya viumbe hai.
Itakumbukwa kuwa Rwanda ilipiga matumizi ya mifuko ya plastiki tangu mwaka 2006, lakini vifaa vingine vya plastiki kama sahani, vijiko na vikombe viliendelea kutumika. Sasa imetangaza kupiga hatua nyingine mbele kufanikisha mkakati huo kwa kupiga marufuku vifaa vyote vya plastiki.
Mwandishi wetu wa Kigali, Sylvanus Karemera ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo.
Tags