Al Sisi aanza mikakati ya kurefusha kipindi cha urais Misri
(last modified Tue, 07 Aug 2018 02:19:09 GMT )
Aug 07, 2018 02:19 UTC
  • Al Sisi aanza mikakati ya kurefusha kipindi cha urais Misri

Rais Abdul Fattah al Sisi wa Misri ameanzisha mikakati ya kurefusha kipindi cha rais wa nchi hiyo kutoka vipindi viwili hadi vitatu.

Kituo cha habati cha al Arabi kimeripoti kuwa, Rais Abdul Fattah al Sisi wa Misri ameanzisha mikakati, kupitia taasisi za serikali, ya kutaka kuzidisha kipindi cha uraia hadi vipindi vitatu. 

Ripoti zinasema kuwa, baadhi ya taasisi na jumuiya za serikali zimewasilisha maombi ya kutaka kuzidishwa vipindi cha urais kutoka viwili vya sasa na kuwa vipindi vitatu. Watu waliotia saini matakwa hayo wanatakiwa kusajili majina na nambari za vitambulisho vyao vya taifa. 

Maombi hayo yanamtaka Abdul Fattah al Sisi abakie madarakani na kugombea kipindi kingine cha tatu. Kwa mujibu wa katiba ya sasa ya Misri, Abdul Fattah al Sisi haruhusiwi kugombea kwa mara ya tatu baada ya kumalizika kipindi chake cha pili cha urais mwaka 2022. 

Maombi hayo yanataka kubadilihwa katiba ya mwaka 2014 ya Misri na kumruhusu al Sisi kugombea kipindi kingine cha tatu. 

Wamisri wameanza kupinga mikakati ya al Sisi ya kurefusha kipindi cha urais

Rais wa Misri anaruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili tu vya miaka minne minne. 

Viongozi wa nchi kadhaa za Afrika kama Rwanda, Uganda na Cameroon wamerefusha kipindi cha uongozi wa rais au kubadilisha katiba kwa shabaha ya kubakia madarakani.

Itakumbukwa kuwa Jenerali mstaafu Abdul Fattah al Sisi alichukua madaraka ya Misri mwaka 2014 baada ya mapinduzi ya jeshi yaliyoindoa madarakani serikali ya kwanza kuchaguliwa kwa njia za kidemokrasia nchini humo. 

Tags