Watoto wa shule ya msingi wasiopungua 22 waaga dunia kufuata kuzama boti Sudan
Aug 16, 2018 02:35 UTC
Watoto wa shule ya msingi wasiopungua 22 jana waliaga dunia baada ya kuzama boti iliyokuwa imepakia watu zaidi ya 40 wakati ikivuka mto Nile kaskazini mwa Sudan.
Jeshi la ulinzi la Sudan limesema, linaendelea na jitihada za kutafuta miili ya watoto walioaga dunia kufuatia ajali hiyo ya boti katika Mto Nile kaskazini mwa Sudan.
Jeshi hilo limeongeza kuwa, injini ya boti ilishindwa kufanya kazi katika mawimbi makubwa ya maji wakati ilipokuwa ikivuka Mto Nile kuelekea katika shule iliyopo katika eneo la Kabna kwenye kijiji kimoja kaskazini mwa Sudan.
Mama mmoja ambaye ameaga dunia katika ajali hiyo ya kuzama boti ametambuliwa kuwa mfanyakazi wa hospitali katika kijiji hicho.