UN: Burundi ingali inatenda jinai dhidi ya binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47919-un_burundi_ingali_inatenda_jinai_dhidi_ya_binadamu
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu iliyotolewa leo inaeleza kuwa jinai zaidi dhidi ya binadamu zimetekelezwa Burundi mwaka 2017 na huu wa 2018.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 05, 2018 09:15 UTC
  • UN: Burundi ingali inatenda jinai dhidi ya binadamu

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu iliyotolewa leo inaeleza kuwa jinai zaidi dhidi ya binadamu zimetekelezwa Burundi mwaka 2017 na huu wa 2018.

Burundi imejaribu na kushindwa kusimamisha tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi iliyoundwa mwaka 2016 na Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo. Kwa upande wake Burundi ilikataa kushirikiana na tume hiyo. Mwaka jana tume hiyo ya uchunguzi ilieleza kuwa maafisa wa ngazi ya juu nchini Burundi walihusika katika jinai hizo dhidi ya binadamu. Ripoti ya leo ya tume hiyo imebainisha kuwa ina sababu za msingi za kuamini kuwa jinai dhidi ya binadamu zinaendelea kutendwa huko Burundi.

Jinai hizo ni pamoja na mauaji, kuwafunga watu jela kinyume cha sheria, utesaji, ubakaji na aina nyingine za udhalilishaji mkubwa wa kijinsia na kuwakandamiza raia kwa sababu za kisiasa. Burundi ilitumbukia katika machafuko ya kisiasa  mapema mwaka 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwa atagombea kiti cha urais kwa muhula mwingine wa tatu; hatua ambayo ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.  

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi