Wanamgambo wanne wauawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Wanamgambo wanne wameuawa waliposhambulia kambi ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Duru za kiusalama nchini humo zimearifu kuwa, wanamgambo wanne wa kundi la waasi wa Mai-Mai waliuawa jana walipofanya shambulizi dhidi ya kambi moja ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, miili ya wanamgambo hao imekutwa katika eneo la Beni mkoani Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Kongo.
Tarehe 22 Septemba pia raia 14 na wanajeshi 4 wa serikali ya Kongo waliuawa katika shambulio lililodaiwa kufanywa na waasi wa Uganda wa ADF.
Makundi yenye silaha yamezidisha mashambulizi yao katika kambi za jeshi la Kongo tangu siku 15 zilizopita. Maeneo ya katikati, mashariki na kaskazini mwa Kongo yamekumbwa na machafuko kwa miaka 20 sasa. Hali hiyo ya mchafukoge imeenea huko Kongo kutokana na kushindwa jeshi la serikali ya Kinshasa na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kukabiliana na makundi ya waasi yanayobeba silaha.