Maandamano makubwa ya kupinga mfumuko wa bei yafanyika Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50227-maandamano_makubwa_ya_kupinga_mfumuko_wa_bei_yafanyika_sudan
Maandamano makubwa ya kulalamikia mfumuko wa bei yamefanyika katika miji kadhaa ya Sudan ambapo waandamaji wakiwa wabeba mabango na maberamu wamepiga nara dhidi ya serikali ya Khartoum.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 17, 2018 10:01 UTC
  • Maandamano makubwa ya kupinga mfumuko wa bei yafanyika Sudan

Maandamano makubwa ya kulalamikia mfumuko wa bei yamefanyika katika miji kadhaa ya Sudan ambapo waandamaji wakiwa wabeba mabango na maberamu wamepiga nara dhidi ya serikali ya Khartoum.

Maandamano hayo ya wanafunzi yamefanyika katika miji miwili ya El-Fasher katika jimbo la Darfur la magharibi mwa Sudan na Damazin makao makuu ya jimbo la Blue Nile kusini mashariki mwa mji mkuu Khartoum.

Vyombo vya usalama vya maeneo hayo vililazimika kuingilia kati na kuwatawanya waandamanaji hao.

Wanafunzi hao waandamanaji ambao idadi yao inakadiriwa kufika 300 walichoma moto matairi na kuni barabarani na hivyo kukwaza shughuli za kawaida kwa masaa kadhaa.

Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan

Maandamano hayo ya kulalamikia kupanda kwa bei za bidhaa yamefanyika katika hali ambayo, maeneo mbalimbali ya Sudan yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa nishati ya mafuta.

Ripoti mbalimbali kutoka Sudan zinasema kuwa, gharama za maisha nchini Sudan zimepanda kwa asilimia 50 na kupelekea kuibuka mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa  hali ambayo imezidisha malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali.

Wimbi hili jipya la maandamano linashuhudiwa katika hali ambayo, miezi michache iliyopita, Sudan ilikumbwa na maandamano makubwa ya nchi nzima baada ya kushadidi mfumuko wa bei.

Ukata uliokuwa ukiikabili serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir uliifanye itangaze kufunga balozi  zake zisizopungua 13 katika mataifa mbalimbali kama moja ya njia za kupunguza gharama.