Oct 15, 2019 13:30 UTC
  • Kesi ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma yaendelea

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema atakata rufaa kufuatia uamuzi wa mahakama kuu kukataa kuzuia daima mashtaka dhidi yake katika kesi ya ufisadi katika mauzo ya silaha zilizokuwa na thamani ya dola bilioni mbili.

Zuma, aliyetawala baina ya 2009-2018, alikuwa anataka upande wa mshtaka uzuiwe kuendeleza kesi dhidi yake ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha na ufisadi katika kununua vifaa vya kijeshi vya Ulaya kwa ajili ya majeshi ya Afrika Kusini katika muongo wa 90. Wakati huo Zuma alikuwa makamu wa rais wa Thabo Mbeki.

Thabo Mbeki

Mshauri wa Zuma wa masuala ya fedha, Schabir Shaikh alishapatikana na hatia ya kujaribu kuomba rushwa kwa niaba ya bwana Zuma kutoka katika kampuni ya silaha za Ufaransa na kosa hilo lilipelekea afungwe jela mwaka 2005.

Kesi dhidi ya Zuma ilifutwa muda mfupi kabla ya kuwania nafasi ya uraisi mwaka 2009.

 

Tags