Watu elfu 5 wafariki dunia kwa Typhoid Kongo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i57707-watu_elfu_5_wafariki_dunia_kwa_typhoid_kongo_dr
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza habari ya kufariki dunia watu elfu tano kutokana na homa ya matumbo (Typhoid) huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Dec 06, 2019 04:01 UTC
  • Watu elfu 5 wafariki dunia kwa Typhoid Kongo DR

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza habari ya kufariki dunia watu elfu tano kutokana na homa ya matumbo (Typhoid) huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ripoti iliyotolewa jana na WHO kuhusu kuenea ugonjwa wa Typhoid duniani imesema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu 2019, kesi zaidi ya laki mbili na 50 elfu za ugonjwa wa Typhoid zimeripotiwa katika sehemu mbalimbali huku zaidi ya watu 5000 wamefariki dunia Kongo DR pekee. Wahanga wakuu wa ugonjwa huo ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani imeongeza kuwa, homa ya matumbo imeenea katika kona zote za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Kwa mujibu wa shirika hilo, miongoni mwa mambo yanayosababisha jambo hilo ni lishe duni na kupungua chanjo ya ugonjwa huo hasa katika mkoa wa Kivu Kaskazini wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao umekumbwa pia na ugonjwa hatari wa Ebola.

Ripoti ya WHO imeongeza kuwa, mwaka jana 2018 ndio uliokuwa mwaka mbaya zaidi ya kuenea ugonjwa wa Typhoid ambao ulizikumba zaidi nchi nne za Afrika za Liberia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Somalia. Nchi ya Ulaya Mashariki iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo mwaka jana kwa mujibu wa ripoti hiyo ya WHO ni Ukraine.