Morocco yalalamikia kutoalikwa Rabat kwenye mkutano wa amani ya Libya
(last modified Mon, 20 Jan 2020 03:04:07 GMT )
Jan 20, 2020 03:04 UTC
  • Morocco yalalamikia kutoalikwa Rabat kwenye mkutano wa amani ya Libya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco amelalamikia kitendo cha kutoalikwa nchi yake kushiriki mkutano wa amani ya Libya mjini Berlin, Ujerumani na akasema vigezo vinavyotumiwa kuchagua nchi kushiriki katika mkutano huo vinaibua maswali mengi.

Nasser Bourita amesema katika mazungumzo na televisheni ya al Jazeera kuwa Morocco ikiwa nchi jirani na Libya imeshangazwa na kutoalikwa kwenye mkutano huo. Bourita ameongeza kuwa moja ya matatizo ya mkutano wa Berlin ni washiriki wa mkutano huo.  

Tunisia pia imekataa mwaliko huo ikilalamimika kwamba imepewa mwaliko huo kwa kuchelewa kwa ajili ya kushiriki katika mkutano huo wa Berlin. 

Kutoalikwa Morocco na kutoshiriki Tunisia ambazo ni nchi jirani na Libya katika eneo la kaskazini mwa Libya katika mkutano wa Berlin na wakati huo huo kualikwa nchi kama Imarati na Uingereza, kunatilia shaka vigezo vilivyotumiwa kuchagua nchi za washiriki katika mkutano huo. 

Pande zinazopigana nchini Libya tarehe 13 mwezi huu wa Januari zilikutana Moscow nchini Russia kwa ajili ya kusaini mapatano rasmi ya usitishaji vita.  Hata hivyo Jenerali Khalifa Haftar kamanda wa wanamgambo wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya, mwishoni mwa mazungumzo hayo alikataa kusaini mapatano hayo.  

Kamanda Khalifa Haftar wa Libya  

Mkutano huo wa Berlin ulimalizika jana kwa pande zote zilizoshiriki kukubaliana juu ya suala la kutouunga mkono au kuusaidia upande wowote kati ya makundi yanayozozana nchini Libya.

Vilevile umeszisitiza udharura wa kudumishwa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya.

 

Tags