Shirila la Mafuta la Taifa Libya lakataa takwa la Marekani
Shirika la Mafuta la Taifa la Libya limekataa takwa la Marekani la kuanza tena shughuli zake na kutangaza kuwa, takwa hilo la serikali ya Washington haliwezi kutekelezwa.
Taarifa iliyotolewa na Shirila la Mafuta la Taifa la Libya sambamba na kukataa takwa hilo la serikali ya Marekani la kuanza kusafirisha tena mafuta ya nchi hiyo nje ya nchi kupitia bandari za mashariki mwa Libya, imesema kuwa: Shughuli za taasisi hiyo zitaanza tena baada tu ya kukomesha hatua zisizo za kisheria.
Ubalozi wa Marekani mjini Tripoli jana Jumanne uliitaka Libya ianze tena kupeleka nje mafuta yake na kuanzisha tena shughuli za Shirika la Mafuta la Taifa.
Vilevile Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, alikuwa ameeleza matumaini kwamba, taasisi za mafuta za Libya zitaanza tena kufanya kazi baada ya mkutano wa amani uliofanyika Berlin nchinii Ujerumani siku chache zilizopita.
Washiriki katika mkutano huo walitoa wito wa kudhaminiwa usalama wa taasisi za mafuta nchini Libya na kupinga aina yoyote ya utumiaji mbaya wa utajiri wa nishati wa nchi hiyo.