Rais wa Senegal ataka kupanuliwa uhusiano wa nchi yake na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i59673-rais_wa_senegal_ataka_kupanuliwa_uhusiano_wa_nchi_yake_na_iran
Rais Macky Sall wa Senegal ametoa mwito wa kuimarishwa uhusiano wa pande mbili wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 11, 2020 07:14 UTC
  • Rais wa Senegal ataka kupanuliwa uhusiano wa nchi yake na Iran

Rais Macky Sall wa Senegal ametoa mwito wa kuimarishwa uhusiano wa pande mbili wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sall alitoa mwito huo jana Jumanne jijini Dakar, wakati akipokea hati ya utambulisho ya balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Senegal, Mohammad Dehshiri.

Rais Sall amesisitizia haja ya kuboreshwa uhusiano wa pande mbili wa Dakar na Tehran katika nyuga mbalimbali, na uliojengeka katika misingi ya kuheshimiana, udugu na urafiki.

Kwa upande wake, balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Senegal, Mohammad Dehshiri amemfikishia Rais Sall ujumbe wa udugu na urafiki kutoka kwa mwenzake wa Iran, Dakta Hassan Rouhani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif alipoitembelea Senegal mwaka jana

Katika ujumbe kwa Rais Sall, Rais Rouhani ameeleza juu ya utayarifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano na nchi hiyo ya Kiafrika katika nyuga za siasa, uchumi, utamaduni, sayansi pamoja na uhusiano wa kibunge.

Naye, Amadou Ba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal ambaye pia alihudhuria hafla hiyo ya jana katika Ikulu ya Senegal, amesema anatumai kuwa balozi mpya wa Iran jijini Dakar atachukua hatua athirifu na amilifu za kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili katika nyanja tofauti.