Ethiopia yaonyesha wasi wasi kufuatia hatua ya Saudia ya kuwatimua Waethopia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60338-ethiopia_yaonyesha_wasi_wasi_kufuatia_hatua_ya_saudia_ya_kuwatimua_waethopia
Serikali ya Ethiopia imeonyesha wasi wasi wake kufuatia hatua ya Saudia ya kuwatimua raia wa nchi hiyo bila ya kuwafanyia vipimo vya Corona.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2020 02:09 UTC
  • Ethiopia yaonyesha wasi wasi kufuatia hatua ya Saudia ya kuwatimua Waethopia

Serikali ya Ethiopia imeonyesha wasi wasi wake kufuatia hatua ya Saudia ya kuwatimua raia wa nchi hiyo bila ya kuwafanyia vipimo vya Corona.

Hivi karibuni gazeti la Financial Times liliripoti kuwa viongozi wa Saudi Arabia wanakusudia kuwafukuza maelfu ya Waethopia ambao ni miongoni mwa wageni wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Corona. Viongozi wa afya nchini Ethiopia wamesema kuwa hatua hiyo ya Riyadh inatia wasi wasi mkubwa. Wasaudia wanadai kuwa wageni hao wanaondoka nchini humo kwa ridhaa yao na baada ya kufuata taratibu za kisheria

Hali mbaya ya Waethiopia huko nchini Saudi Arabia

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya Ethiopia, hadi sasa watu 71 wameathirika virusi vya Corona ambapo kati yao watu 10 wamepoteza maisha. Itakumbukwa kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 viliibuka kwa mara ya kwanza mwezi Disemba mwaka jana katika mji wa Wuhan nchini China na hadi sasa vimeenea katika zaidi ya nchi 200 za dunia. Hadi sasa zaidi ya watu milioni moja na laki nane na elfu 53 duniani, wameathirika virusi hivyo, huku watu laki moja na elfu 14,247 wakiwa wamepoteza maisha.