Wasi wasi wa WHO kuhusu kuenea kimya kimya COVID-19 barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61225-wasi_wasi_wa_who_kuhusu_kuenea_kimya_kimya_covid_19_barani_afrika
Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema ingawa Afrika ndilo eneo ambalo lina idadi ndogo zaidi ya waathirika wa ugonjwa wa COVID-19 lakini kuna wasi wasi kuwa ugonjwa huo utaenea kimya kimya iwapo viongozi wa bara hilo hawatalipa umuhimu suala ya vipimo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 26, 2020 05:50 UTC
  • Wasi wasi wa WHO kuhusu kuenea kimya kimya COVID-19 barani Afrika

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema ingawa Afrika ndilo eneo ambalo lina idadi ndogo zaidi ya waathirika wa ugonjwa wa COVID-19 lakini kuna wasi wasi kuwa ugonjwa huo utaenea kimya kimya iwapo viongozi wa bara hilo hawatalipa umuhimu suala ya vipimo.

Mjumbe wa WHO Samba Sow ametahadahrisha kuwa ukosefu wa vipimo huenda ukapelekea janga la COVID-19 kuenea kimya kimya barani Afrika na hivyo viongozi wa bara hilo wanapaswa kulipa kipaumbele suala la vipimo.

Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC), hadi kufikia Mei 26 idadi ya waliofariki kutokana na COVID-19 barani Afrika walikuwa ni 3,471.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliofariki ni rais wa zamani wa Jamhuri ya Congo Jacques Joachim Yhombi-Opango na Waziri Mkuu wa zamani wa Somalia Nur Hassan Hussein. Aidha kwa mujibu wa takwimu hizo idadi ya walioambukizwa COVID-19 barani Afrika ni 115,346 huku 46,426 wakipona baada ya kupata matibabu.

Wataalamu wanaonya kuwa, iwapo ugonjwa huo utaenea sana Afrika basi bara hilo litashindwa kukabiliana na hali hiyo kutokana na mifumo dhaifu ya afya.