Miili ya watu 40 waliouliwa mapiganoni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yapatikana
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i62421-miili_ya_watu_40_waliouliwa_mapiganoni_jamhuri_ya_kidemokrasia_ya_kongo_yapatikana
Duru za habari za ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeripoti kuwa miili ya watu 40 imegunduliwa nchini baada ya kujiri mapigano kati ya makundi mawili yenye silaha.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jul 25, 2020 22:49 UTC
  • Miili ya watu 40 waliouliwa mapiganoni  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yapatikana

Duru za habari za ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeripoti kuwa miili ya watu 40 imegunduliwa nchini baada ya kujiri mapigano kati ya makundi mawili yenye silaha.

Duru hizo jana Jumamosi zilitangaza kuwa miili hiyo imepatikana tangu Alhamisi iliyopita katika eneo la Pinga mkoani Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Kongo ambalo katika siku ya karibuni limeshuhudia mapigano ya umwagaji damu kati ya makundi mawili ya wanamgambo hasimu.

Eneo la Pinga kulikopatikana miili ya watu 40 waliouliwa mapiganoni 

Wanajeshi watano na raia 12 waliuliwa katika mapigano hayo; na kuna uwezekano mkubwa miili iliyosalia pia ni ya wanamgambo. 

Mapigano hayo yamejiri kati ya kundi la wanamgambo kwa jina la NDC-R linaloongozwa na Guidon Shimirai Mwissa ambaye anasakwa na mahakama za Kongo tangu mwaka 2018, na kundi lenye silaha  linaloongozwa na mmoja wa wanachama wa watajika wa kundi hilo la NDC-R. 

Itakumbukwa kuwa, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hivi karibuni lililikomboa eneo la Pinga kutoka mikononi mwa makundi ya wanamgambo. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa mikoa ya Ituri, Kivu ya Kaskazini na Kivu Kusini yamekuwa yakikabiliwa zaidi ya hali ya mchafuko na mapigano ikilinganishwa na maeneo mengine ya nchi hiyo.