Alassane Ouattara kugombea kiti cha urais Kodivaa kwa mara ya tatu
-
Alassane Ouattara
Mkutano wa kumuarifisha Alassane Ouattara kama mgombea wa kiti cha rais katika uchaguzi ujao nchini Ivory Coast umefanyika katika mji wa nchi hiyo, Abdijan.
Katika mkutano huo uliofanyika jana Jumapili ukihudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa Alassane Ouattara, kiongozi huyo amesisitiza udhafura wa kupata ushindi katika ujao wa rais.
Vyama vya upinzani na jumuiya za kiraia nchini Ivory Coast zimepinga hatua ya Ouattara kugombea kiti cha rais kwa mara ya tatu. Hata hivyo Alassane Ouattara mwenyewe na chama tawala cha RHDP wanaamini kuwa, "Jamhuri ya Tatu" imeanza nchini humo na kwamba yeye ni mgombea wa kwanza katika jamhuri hiyo ya Ivory Coast baada ya kufanyiwa marekebsho katiba ya nchi mwaka 2016.
Henri Konan Bedie mwenye umri wa miaka 87 ambaye ndiye Spika wa Bunge la Ivory Coast na rais wa zamani wa Ivory Coast pia anagombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini humo.