Hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe yazidi kuzorota
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63976-hali_ya_kiafya_ya_sheikh_ibrahim_zakzaky_na_mkewe_yazidi_kuzorota
Binti wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, hali ya kiafya ya baba na mama yake ni mbaya mno kutokana na kiongozi huyo kuzuiawa kupatiwa matibabi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 12, 2020 13:29 UTC
  • Hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe yazidi kuzorota

Binti wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, hali ya kiafya ya baba na mama yake ni mbaya mno kutokana na kiongozi huyo kuzuiawa kupatiwa matibabi.

Suhaila Zakzaky ameeleza kuwa, wakati baba na mama yake walipotiwa mbaroni walikuwa wamejeruhiwa kwamba, hivi sasa hali yao ya kiafya imezidi kuwa mbaya kutokana na kuzuiwa kupatiwa matibabu na huduma nyingine muhimu.

Suhaila ameongeza kusema kuwa, hadi sasa baba yake akiwa gerezani amepata mshtuko wa ubongo mara mbili huku akiwa pia na sumu kwenye damu sambamba na mada ya risasi mambo ambayo yanatishia uhai wake.

Aidha amesema, mama yake pia ambaye alijeruhiwa kwa risasi tano, alipaswa kufanyiwa operesheni lakini hadi sasa hilo halijafanyika na hivyo ameendelea kuteseka kwa maumivu makali.

Suhaila Zakzaky, binti ya Sheikh Ibrahim Zakzaky

 

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi katika shambulio hilo.

Mahakama Kuu ya Nigeria iliwahi kutoa hukumu iliyosisitiza kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe hawana hatia yoyote na ikaamuru waachiliwe huru, lakini wawili hao wangali wanaendelea kushikiliwa jela.

Wakati huo huo, hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi.