Rwanda: Kongamano la uchumi Kigali kuangazia teknolojia na mfumo wa dijitali
Rwanda inatazamiwa kuwa mwenyeji wa duru ya 26 ya Kongamano la Uchumi Duniani WEF mapema wiki ijayo. Marais, wajasiriamali na wawekezaji zaidi ya 1,200 wa bara hilo wanatazamiwa kushiriki kongamano hilo litakalofanyika Kigali kati ya Mei 11 na 13.
Mbali na maswala ya ushirikiano katika uga wa uchumi-jamii miongoni wa nchi za Afrika, kongamano hilo linataziwa kujikita pia katika swala la teknolojia na mfumo wa dijitali.
Elsie Kanza, Mkuu wa Kamati Kuu inayoandaa kongamano hilo amesema: "Mkutano huo wa wiki ijayo utajikita zaidi kuhusu ni jinsi gani taasisi za nchi za Kiafrika zitaimarisha huduma na utendaji kazi wao kwa kutumia mifumo ya kisasa ya teknolojia.
Kwa upande wake, Claver Gatete, Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda amesema kongamano hilo litatoa fursa ya kutangamana na kubadilishana mawazo wawekezaji wa umma na binafsi.
Mbali na kongamano hilo, Rwanda inatazamiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika AU baadaye mwaka huu. Hayo yalibainika baada ya kutiwa saini mapatano baina ya Balozi wa Rwanda nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika Hope Tumukunde na Djeneba Diarra Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika Mei 4.