Wacongo waliokimbia volcano Goma wanasumbuliwa na ubaha wa chakula, maji
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i70676-wacongo_waliokimbia_volcano_goma_wanasumbuliwa_na_ubaha_wa_chakula_maji
Wakazi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) waliokimbia makazi na nyumba zao Jumamosi iliyopita kutokana na mlipuko wa volkano ya Mlima Nyiragongo ambao wanahofia kutokea mlipuko mwingine wa volkano, wasumbuliwa na uhaba wa chakula na maji.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2021 07:42 UTC
  • Wacongo waliokimbia volcano Goma wanasumbuliwa na ubaha wa chakula, maji

Wakazi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) waliokimbia makazi na nyumba zao Jumamosi iliyopita kutokana na mlipuko wa volkano ya Mlima Nyiragongo ambao wanahofia kutokea mlipuko mwingine wa volkano, wasumbuliwa na uhaba wa chakula na maji.

Makumi ya watu walifariki dunia wakati volkano ya Mlima Nyiragongo, ambayo ni miongoni mwa volkani hai zaidi dunia, iliporipuka wiki moja iliyopita na kumwaga lava katika vitongoji vya kandokando ya mji wa Goma. Mlipuko wa volkano hiyo pia umesababisha uharibifu wa maelfu ya nyumba. Maelfu ya watu walikimbia makazi yao Alhamisi wiki hii wakati serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipoonya kwamba, volkano ya Mlima Nyiragongo inaweza kulipuka tena wakati wowote.

Jumamosi ya leo, mlipuko mdogo ulishuhudiwa katika volkano ya karibu na Mlima Nyamuragira lakini serikali ya DRC inasema si tishio kwa makazi ya watu wa eneo hilo.

Maelfu ya watu wamekimbia nyumba zao Goma kwa hovu ya volkano

Watu wengi wameelekea katika mji wa Sake ulioko kwenye mpaka wa Congo na Rwanda huko Kaskazini Mashariki, wakati wengine wamevuka Ziwa Kivu kwa boti na kuelekea Bukavu. Gavana Theo Ngwabidje wa mkoa wa Kivu Kaskazini amesema karibu watu 10,000 wamekimbilia Bukavu na kwamba wengi wao wamepokewa na familia zao. 

Ijumaa ya jana Rais wa Rwanda, Paul Kagame, aliomba msaada wa haraka wa kimataifa ili kudhibiti mgogoro wa wakimbizi hao. Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) pia umesema watu wapatao 400,000 wanahitaji himaya au ulinzi.