Mwinyi: Zanzibar ipo tayari kupokea chanjo ya COVID-19
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i70898-mwinyi_zanzibar_ipo_tayari_kupokea_chanjo_ya_covid_19
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali iko tayari kupokea msaada wa chanjo ya COVID -19 na misaada mbalimbali ya kitabibu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 04, 2021 14:10 UTC
  •  Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi
    Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali iko tayari kupokea msaada wa chanjo ya COVID -19 na misaada mbalimbali ya kitabibu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).

Dk. Mwinyi amesema hayo Ieo Ikulu Jijini Zanzibar, alipokutana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani, anayefanyia shughuli zake nchini Tanzania Dr. Tigest Ketsela Mengestu.

Amesema sekta ya afya huko Zanzibar ina mahitaji makubwa ili iweze kufanikisha lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo azma ya WHO kuendelea kuisadia Zanzibar katika nyanja mbalimbali, ikiwemo utoaji wa mafunzo kwa madaktari na wafanyakazi wa afya pamoja na uimarishaji wa miundombinu, ni jambo muhimu.

Alisema katika hatua ya kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi, kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo Bima ya Afya nchini.

Aidha, alisema kuna haja ya kuimarisha miundombinu ya huduma za afya, hususan katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja ambayo hivi sasa haikidhi mahitaji katika utoaji wa huduma kutokana ongezeko la watu pamoja na ufinyu wa nafasi.

Alisema Hospitali hiyo yenye majengo ya kale, ni ndogo na ina vyumba vichache vya upasuaji hususan kwa magonjwa makubwa kama vile moyo pamoja na kuwa na wodi chache za kulaza wagonjwa.

Rai Samia Suluhu Hassan akiokea ripoti ya corona kutoka kwa Prof. Said Aboud

Mwezi uliopita wa Mei Kamati ya COVID-19 iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania iliishauri serikali ya nchi hiyo kutoa takwimu za wagonjwa wa corona kwa wananchi na kwa Shirika la Afya Duniani, WHO. Kamati hiyo pia iliishauri serikali kufungua njia za matumizi ya chanjo za COVID-19 ikitumai kuwa hatua hizo zitaisaidia Tanzania kupambana na maambukizo ya ugonjwa huo ambao ni janga la dunia nzima.