Algeria yaipokonya leseni televisheni ya Saudia kwa 'upotoshaji'
(last modified Sun, 01 Aug 2021 08:02:51 GMT )
Aug 01, 2021 08:02 UTC
  • Algeria yaipokonya leseni televisheni ya Saudia kwa 'upotoshaji'

Serikali ya Algeria imeipokonya kanali moja ya televisheni ya Saudi Arabia leseni ya kuhudumu nchini humo.

Wizara ya Habari ya Algeria imesema hatua ya kuifungia kanali ya habari ya Al-Arabia inayomilikiwa na Saudia imetokana na kitendo chake cha kurusha hewani habari za upotoshaji juu ya matukio ya kisiasa yanayoendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Taarifa ya wizara hiyo imesema, Algiers imeipokonya kanali ya Al-Arabia leseni ya kuhudumu nchini humo kwa kutosheshimu maadili ya utangazaji, kurusha hewani habari za upotoshaji na unafiki.

Msemaji wa Serikali na pia Waziri wa Habari wa Algeria, Ammar Belhimer 

Gazeti la  Al-Quds Al-Arabi linalochapishwa kwa lugha ya Kiarabu limeripoti kuwa, taarifa ya Wizara ya Habari ya Algeria haijatoa maelezo zaidi na ya kina juu ya uamuzi wake huo, ghairi ya kuituhumu televisheni hiyo ya satalaiti ya Riyadh kwa upotoshaji na unafiki.

Haya yanajiri miezi michache baada ya nchi hiyo ya Kiarabu kuifungia kanali ya televisheni ya Ufaransa ya France 24 kutokana na kile kilichotajwa kuwa hatua yake ya kukariri wazi wazi uhasama dhidi ya taifa hilo na taasisi zake.

 

Tags