UN yatahadharisha: Madagascar inakaribia kukumbwa na njaa kutokana na ukame mkubwa
(last modified Fri, 03 Sep 2021 11:43:02 GMT )
Sep 03, 2021 11:43 UTC
  • UN yatahadharisha: Madagascar inakaribia kukumbwa na njaa kutokana na ukame mkubwa

Kisiwa cha Madagascar kinachopatikana katika Bahari ya Hindi barani Afrika kwa miaka minne sasa kimeathiriwa na ukame uliosabbaishwa na mabadiliko ya tabianchi. Watu nchini humo wanalazimika kula nzige na majani ya mwituni ili kubakia hai.

Mpango wa Chakuka wa Umoja wa Mataifa (WFP) umeripoti kuwa, Madagascar kwa muda mrefu sasa imekumbwa na ukame na mafuriko na kwamba ukame wa karibu miaka minne ulioiathiri nchi hiyo umepelekea watu wasiopungua elfu 30 kukabiliwa na ukosefu wa chakula. 

Njaa yawaathiri wananchi wa Madagascar 

Umoja wa Mataifa umesema, watu zaidi ya milioni 1.1 huko Madagascar wanasumbuliwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula na wanahitaji misaada ya haraka.

Wakati huo huo taathira za ukame zimedhoofisha kilimo kwa asilimia karibu 60 katika aghalabu ya mikoa yenye idadi kubwa ya watu nchini humo. Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu maafa makubwa ya binadamu huko Madagascar kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kula nzige, majani ya mwituni, tope na matunda ya cactus ili kuweza kuishi. 

Msemaji wa WFP, Shelley Thakral ameeleza kuwa, ukame umewaathiri sana wananchi wa Madagascar na kwamba ni mwaka wa nne sasa ambapo wakulima nchini humo wanasubiri kupata mavuno angalau kidogo. Amesema hali hiyo imezidishwa na janga la COVID-19. kwa kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakitafura ajira za msimu kipindi cha utalii, hata hivyo hakuna watalii wanaoelekea Madagascar kwa miezi 18 sasa kutokana na maambukizi ya COVID-19. 

Tags