May 21, 2016 15:57 UTC
  • Waasi kadhaa watiwa mbaroni mashariki mwa DRC

Afisa mmoja mwandanamizi wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametangaza habari ya kutiwa mbaroni waasi kadhaa wa kundi la Mai Mai, mashariki mwa nchi hiyo.

André Ehonza, kamanda wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, waasi wawili wa kundi la Mai Mai ni miongoni mwa waasi waliotiwa mbaroni katika operesheni maalumu iliyofanywa na jeshi katika eneo la Uvira, la mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

André Ehonza ameongeza kuwa, tangu siku kumi zilizopita, jeshi la Kongo limefanya opereseheni nyingi katika eneo la Kigushu la Kivu Kusini.

Ikumbukwe kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016 hadi hivi sasa waasi wa Mai Mai wamefanya uhalifu mbalimbali kama vile mauaji, kuteka nyara watu, kunajisi, kupora, wizi na kuchoma moto nyumba za raia huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Duru za eneo hilo zinasema kuwa, magenge yenye silaha ndiyo wavunjaji wakuu wa usalama mashariki mwa Kongo kwa muda wa miaka 20 sasa.

Jeshi la serikali na asakari wa kofi buluu wa Umoja wa Mataifa wameshindwa kukabiliana na wanamgambo wanaofanya uhalifu katika maeneo tofauti ya nchi hiyo kubwa ya katikati mwa Afrika.

Tags