Idadi ya wagombea urais wa Kongo Brazzaville yaongezeka
Wapinzani wengine wawili wa serikali ya Jamhuri ya Kongo wametangaza kuwa watagombea katika uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika tarehe 20 ya mwezi ujao wa Machi.
Clément Miérassa ambaye ni mwanasiasa wa chama cha Demokrasia ya Kijamii amesema, kwa kuzingatia mazingira yaliyopo kuna udharura wa wapinzani wa serikali kugombea katika uchaguzi wa rais ili kuleta mabadiliko nchini.
Guy-Brice Parfait Kolélas amesema japokuwa mazingira yaliyopo hayaridhishi kwa ajili ya kufanya uchaguzi lakini atashiriki kwenye kinyang'anyiro hicho.
Awali muungano mkuu wa upinzani nchini Kongo Brazzaville uitwao Muungano wa Afrika kwa ajili ya Demkrasia ya Kijamii ulimtangaza Pascal Tsaty Mabiala kuwa mgombea wake katika uchaguzi ujao wa rais.
Uchaguzi wa rais wa Kongo Brazzaville ulikuwa ufanyike mwezi Julai, lakini tarehe yake ikarejeshwa nyuma na Rais wa nchi hiyo Denis Sassou Nguesso kuwa tarehe 20 ya mwezi ujao wa Machi.../