Zimbabwe yaanza kutwaa tena ardhi ambazo hazijatumika kutoka kwa wakulima wazawa
(last modified Thu, 31 Mar 2022 10:16:47 GMT )
Mar 31, 2022 10:16 UTC
  • Zimbabwe yaanza kutwaa tena ardhi ambazo hazijatumika kutoka kwa wakulima wazawa

Zimbabwe imeanza kitwaa tena ardhi za kilimo kutoka kwa raia asili na weusi wa nchi hiyo ambazo walipewa chini ya mpango wa mageuzi makubwa ya ardhi yaliyofanywa wakati wa utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe miongo miwili iliyopita lakini walizitelekeza bila kuzitumia.

Haya yameelezwa na Anxious Masuka, Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe. Amesema, mpango huo utawalenga wananchi ambao mashamba yao hayatumiki na wale wanaomiliki mashamba mengi nchini humo. Amesema baada ya kuzitwaa ardhi hizo za kilimo, mashamba hayo yatagawiwa kwa wakulima waliopo kwenye orodha ya wanaosubiri ambao walisalia katika  awamu za awali za mageuzi ya ardhi huko Zimbabwe.

Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe ameongeza kuwa, nchi hiyo ina nafasi finyu ya kijiografia na kwamba ardhi ambayo inayogawiwa inayochukuliwa kutoka kwa raia weusi wa nchi hiyo na kuigawa kwa wengine kama hao. Mashamba ya wazawa ambayo yamelimwa hayataguswa katika mpango huo. 

Mwaka 2000 rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe alianzisha mpango wa mageuzi ya ardhi ambapo wakulima wazungu waliondolewa kwa nguvu kwenye ardhi walizokuwa wakizimiliki na kisha serikali ikazigawa ardhi hizo za kilimo kwa raia asili wa Zimbabwe. 

Ardhi zisizozimwa kutwaliwa na serikali ZImbabwe