Sudan Kusini yatangaza kutuma wanajeshi 750 mashariki mwa Kongo
Sudan Kusini imetangaza kutumwa wanajeshi wake 750 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Akizungumza katika hafa ya kuwaaga wanajeshi hao huko Juba, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amewahimiza askari hao kutii sheria na kuwalinda raia.
Mapigano makali katika miezi ya karibuni kati ya jeshi la Kongo na waasi wa kundi la M23 yameipelekea Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutumwa kikosi cha kikanda cha askari jeshi wa kudumisha amani kinachojumuisha wanajeshi kutoka Kenya, Burundi na Uganda.
Akizungumza mbele ya wanajeshi hao, Rais Kiir amesema hivi na hapa nimanukuu:" hivi sasa nyie ni kikosi kilichojipanga na mnaenda kudumisha amani ingawa hamjavaa kofi za bluu ambazo kwa kawaida huvaliwa na askari jeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa; lakini kofia mnazovaa sasa zitabadilika na kuwa bluu kulingana na utendaji wenu.," mwisho wa kunukuu. Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Sudan Kusini amesisitiza kwa mara nyingine tena umuhimu wa misheni hiyo ya askari jeshi wa nchi hiyo mashariki mwa Kongo.
Angelina Teny amebainisha hivi na ninamnukuu " tangu Sudan Kusini ipate uhuru huu ni ujumbe wa kwanza wa nchi hiyo kushiriki katika kikosi cha kikanda kwa lengo la kulinda amani; na ni muhimu sana kwa sababu nchini kwetu tuna walinda amani kwa ajili ya kuwalinda raia lakini sasa tunakwenda kurejesha amani na uthabiti na kurejesha amani kamili huko Kongo na katikamipaka yetu yote', mwisho wa kunukuu.
Sudan Kusini imetangaza kutuma wanajeshi mashariki mwa Kongo miezi minne baada ya maelfu ya wapiganaji wakiwemo waasi wa zamani watiifu kwa Kiir na makamu wake Riek machar kuunganishwa katika jeshi la taifa la Sudan Kusini. Kuunganishwa wapiganaji hao jeshi lilikuwa sharti muhimu kwa mapatano ya amani yaliyofikiwa na pande mbili ili kuhitimisha vita vya ndani nchini humo.