Jan 25, 2023 03:03 UTC
  • Madagascar yakumbwa na tufani ya Cheneso;  barabara kuelekea mji mkuu zimebomoka

Wilaya kadhaa katika mkoa wa Mahajanga kaskazini magharibi mwa Madagascar zimekumbwa na mafuriko pamoja na barabara zinazoziunganisha wilaya hizo kueleke amji mkuu, Antananarivo. Kimbunga kwa jina la "Cheneso" kinaendelea kukiathiri kisiwa hicho kinachopatikana katika bahari ya Hindi huku watu zaidi ya 15,000 pia wakiathirika.

Bonne Fehy mmoja kati ya watu walioathirika na mafuriko kuafuatia kimbunga cha Cheneso huko Madagascar ameeleza kuwa na hapa ninamkuu "nimelazimika kuiacha nyumba yangu kwa sababu iliharibiwa na upepo mkali wa kimbunga, vitu vyote vyetu vimerowa maji," mwisho wa kunukuu. 

Mbali na mafuriko hayo tajwa, Ofisi ya Taifa ya Kushughulikia Maafa na Majanga ya Kimaumbile ya Madagascar imesajili matukio kadhaa ya maporomo ya udongo hadi sasa.  Olga Rasoanirina Mkurugenzi wa mkoa wa Boeny ameeleza kuwa, wametoa makazi kwa watu kadhaa walioathiriwa na kimbunga cha Cheneso tangu Jumapili iliyopita wakati kulipotokea upepo mkali. Amesema wameandaa maeneo katika shule moja ya serikali ambapo waathirika wa mafuriko wanapatiwa huduma ikiwemo chakula. 

Hadi kufikia sasa watu 4 wameripotiwa kuaga dunia, 14 hawajaulikani walipo na wengine zaidi ya 8000 wameathirika na kimbunga cha Cheneso kilichoikumba Madagascar. 

 

Tags