Mar 08, 2023 03:01 UTC
  • UNICEF: Mlipuko wa kipindupindu unatishia maisha ya watoto nchini Malawi

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) imesema kufikia tarehe 26 Februari mwaka huu, kesi 48,815 za kipindupindu na vifo 1,5471 vimesajiliwa nchini Malawi. Ripoti hiyo imesema kesi 12,293 na vifo 203 kati ya watoto ziliripotiwa kwa jumla nchini Malawi kufikia Februari 19, 2023.

UNICEF imetangaza kuwa, karibu watoto milioni 4.8 nchini Malawi, au mmoja kati ya wawili, wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu nchini Malawi katika rekodi umesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500, wakiwemo watoto 197, tangu mwezi Machi 2022.

Mlipuko huo ulitangazwa kuwa dharura ya afya ya umma na serikali ya Malawi mnamo Desemba 5 mwaka jana. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasaidia mamlaka, hasa kwa kutoa vifaa vya matibabu na kuongeza uwezo wa kupima.

Ripoti iliyotolewa na mjini Geneva imesema: “Kuwa na mtoto mwenye utapiamlo mkali ana uwezekano wa kufa kwa kipindupindu mara 11 zaidi ya mtoto mwenye lishe bora, na kwamba mlipuko wa kipindupindu unaweza kuwa hukumu ya kifo kwa maelfu ya watoto nchini Malawi,”.

Riipoti ya UNICEF imesema Malawi inakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu katika historia yake. Nchi hiyo pia inasumbuliwa na mlipuko wa polio na kesi zinazoendelea za maambukizi ya COVID-19 kote nchini.

UNICEF imezipa kipaumbele wilaya sita kulingana na idadi kubwa ya vifoambazo ni Lilongwe, Mangochi, Blantyre, Balaka, Salima, na Machinga.

Tags